Tshishimbi apongeza usajili wa nyota wapya Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Jan 2020
Tshishimbi apongeza usajili wa nyota wapya Yanga

Achana na matokeo ya mchezo wa jana Jumatano kati ya Yanga na Kagera Sugar, nahodha wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi ameibuka na kuupongeza uongozi wao kwa kufanya usajili matata kwenye dirisha dogo.

Mcongomani huyo anaamini ujio wa nyota wapya waliosajiliwa dirisha dogo, umeongeza uhai na kuziba nafasi zilizoachwa wazi huku akiweka wazi kwamba, nafasi ya kufanya kweli iko wazi na msimu ujao watashiriki michuano ya kimataifa.

Alisema kulikuwa na kina Juma Balinya, Issa Bigirimana, Mayben Kalengo, David Molinga na nyota wengine baada ya kutimuliwa kwao hakuna kinachokumbukwa kutokana na kutua kwa nyota wapya wakali zaidi.

"Usajili uliofanya unahitaji kutoa pongezi kwa viongozi kwani wamefanya kitu ambacho kimerudisha heshima ya klabu wachezaji waliosajiliwa hasa waliopata nafasi ya kucheza kama Ditram Nchimbi, Haruna Niyonzima, Adeyum Salum na Tariq Seif wameonyesha viongozi hawakukosea kuwasajili," Tshishimbi aliiambia Mwanaspoti

"Tunatakiwa kuwapa muda, nategemea watafanya kitu kikubwa zaidi kikubwa ni uongozi kuendelea kuwatengenezea mazingira mazuri ili waendelee kufanya vitu bora zaidi na kuweza kuifanya timu ikiwapa changamoto wapinzani wetu kwenye kila mashindano tutakayoshiriki," alisema.

Tshishimbi aliongeza kwa kuzungumzia suala la kocha mpya Luc Eymael ambapo alifunguka kuwa ujio wake umeongeza changamoto ya wachezaji kupambana lengo likiwa ni kuonyesha nini wanacho ili kujitengenezea mazingira ya kupata namba kikosi cha kwanza.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
7h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
19h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’