Kocha mkuu wa Yanga George Lwandamina, amesema kikosi chake kinakwenda kukutana na Simba Jumamosi, ijayo akiwa na uhakika wa ushindi kutokana na kiwango na ubora waliokuwa nao hivisasa.
Kocha huyo asiye na maneno mengi amesema ushindi walioupata dhidi ya Stand United umeongeza matumaini ya kuibuka na ushindi katika mchezo huo ambao amesema ndiyo utakao warudisha kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Vodacom inayoendelea hivisasa.
"Tupo imara na timejipanga kuhakikisha tunashinda mchezo wetu wa Jumamosi ni mchezo mgumu lakini naamini hakuna kitakachoshindikana kutokana na ubora tuliokuwa nao kwasasa," amesema Lwandamina.
Kocha huyo amesema kitendo cha kwenda kwenye mchezo huo wakati wanalingana kwa pointi na vinara hao kimemwongezea ari na ujasiri wakwenda kupambana na kupata matokeo ya mchezo huo na anaamini hilo litatokea kutokana na mikakati waliyokuwa nayo kuelekea mchezo huo.
Kocha huyo raia wa Zambia amesema wameupa umuhimu mkubwa mchezo huo lengo ni kuhakikisha wanakaa kileleni kwa tofauti ya pointi na siyo mabao kama ilivyokuwa sasa ambapo Simba wanaongoza kwa wingi wa mabao na siyo pointi.
Yanga na Simba kwasasa zipo katika nafasi ya juu zote zikiwa na pointi 15, lakini Simba ndiyo ipo kwenye nafasi ya kwanza kutokana na idadi kubwa ya mabao ya kufunga iliyokuwa nayo.
Kama Yanga itaibuka na ushindi katika mchezo huo, utakuwa ushindi kwa kwanza wa Lwandamina dhidi ya Simba tangu ajiunge na Yanga mwaka mmoja uliopita

ADVERTISE HERE