Eymael ataka ushindi dhidi ya Azam Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Jan 2020
Eymael ataka ushindi dhidi ya Azam Fc

Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa kesho Jumamosi kwenye uwanja wa Taifa hautakuwa mwepesi

Mbelgiji huyo amesema ameifuatilia Azam Fc na kubaini wana timu nzuri hivyo anatarajia upinzani mkali

"Tunatarajia upinzani mkali kutoka kwa Azam Fc kwani nimewaona, wana timu nzuri. Sisi tumefanya maandalizi ya kutosha, tunahitaji kushinda mchezo huo," amesema

"Jioni tutafanya maandalizi ya mwisho, nilipenda tufanye mazoezi usiku kwenye uwanja wa Taifa lakini hatukuruhusiwa. Tutafanya mazoezi mepesi na kuwapa maelekezo ya mwisho wachezaji"

Huo utakuwa mchezo wa pili kwa Eymael tangu alipojiunga na Yanga akipoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Kagera Sugar kwa kufungwa mabao 3-0

Eymael anahitaji kupata matokeo ya ushindi kwenye mchezo huo kwani kama Yanga itafungwa huenda akajikuta kwenye wakati mgumu mapema sana

Viingilio vya mchezo huo VIP A ni Tsh 15,000/-, VIP B na C ni Tsh 10,000/- na Mzunguuko ni Tsh 5,000/-

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’