Sasii kuchezesha mpambano wa watani wa Jadi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Oct 2017
Sasii kuchezesha mpambano wa watani wa Jadi
Mwamuzi Bora wa msimu uliopita, Elly Sasii ndiye aliyeteuliwa kuchezesha pambano la watani wa jadi nchini, Simba na Yanga litakalopigwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Uhuru

Kwa mujibu wa chanzo kutoka ndani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), mwamuzi huyo kijana ndiye atakayepuliza kipyenga katikati ya Uwanja wa Uhuru na kusaidiwa na washika vibendera Joseph Bulali na Sudi Lila, huku mezani akiwa mkongwe, Israel Nkongo.

Simba na Yanga zinatarajiwa kuvaana katika pambano lao la kwanza la Ligi Kuu Bara msimu huu, linalokuwa la 99 kwa timu hizo kukutana katika ligi tangu mwaka 1965.

Sasii ndiye aliyechezesha pambano la Ngao ya Jamii kati ya Simba na Yanga lililochezwa Agosti 20 kwenye Uwanja wa Taifa na Yanga kulala kwa mikwaju ya penalti 5-4 baada ya dakika 90 za mchezo huo kumalizika kwa suluhu.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
12m ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
3h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
12h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’