Kiungo Mnyarwanda Haruna Niyonzima jana aliifungia Yanga bao lake la kwanza tangu arejee kwa mabingwa hao wa kihistoria usajili wa dirisha dogo
Niyonzima alionyesha uwezo mkubwa katika mchezo huo dhidi ya Singida United ambao Yanga iliondoka na ushindi wa mabao 3-1
Akizungumza baada ya mchezo huo, Niyonzima alisema matokeo hayo ni ishara kuwa timu yao imeanza kuwa sawa
"Hatukupata ushindi kwenye michezo mitatu iliyopita lakini sababu kubwa ni kuwa wachezaji hatukuwa tumezoeana. Timu yetu ni mpya, ina koicha mpya na wachezaji wengi wapya"
"Lakini nisema tu sasa tumaenza kuwa sawa, naamini baada ya muda tutakuwa na timu nzuri sana. Kikubwa nawaomba viongozi, wanachama, mashabiki pamoja na wadhamini wetu GSM waendelee kuwa pamoja nasi ili kuhakikisha tunatimiza malengo yetu"
Tangu arejee Yanga, Niyonzima amecheza mechi zote nne za ligi