Yanga yamkomalia Ali Ali, mwenyewe ataka mkataba uvunjwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Jan 2020
Yanga yamkomalia Ali Ali, mwenyewe ataka mkataba uvunjwe

Uongozi wa klabu ya Yanga umemsisitizia beki wake Ali Ali kuwa anapaswa kujiunga na JKT Tanzania alikopelekwa kwa mkopo

Inaelezwa Ali aliyetua Yanga kutoka klabu ya KMC, ameondolewa kwenye kikosi cha Yanga na anapaswa kwenda kuitumikia JKT Tanzania

Aidha huyo beki hodari wa kupiga mipira ya vichwa, aliomba apelekwe klabu ya KMC, hata hivyo ombi hilo lilikataliwa

Ali ameweka msimamo wa kutojiunga na JKT Tanzania na sasa akiutaka uongozi wa Yanga uvunje mkataba wake

Alichosema kuhusu sakata lake;

"Dirisha lilikuwa linafungwa usiku halafu siku hiyo hiyo nikaambiwa naenda kwa mkopo JKT Tanzania, nilikataa nikawaambia nitabaki hapa hapa nitapambana kuhakikisha napigania namba kwa kuwa nina uwezo, Katibu akanijibu sawa"

"Baada ya hapo nikaona taarifa nimetolewa kwa mkopo, nikawasiliana na Katibu akanijibu ni lazima niondoke kwa mkopo

"Nikampa masharti nitolewe kwa mkopo kwenda KMC lakini Yanga SC wakakataa Nilimuuliza katibu sijui hatma yangu kwa kuwa wenzangu walikuwa Singida na mimi nipo njia panda

"Kiukweli sitoweza kuwasiliana naye tena kutokana na majibu aliyonipa ila akanisisitiza siwezi kujiunga na Yanga tena. Kama Yanga hawanitaki ni vema wakavunja mkataba wangu niwe huru kwa maana sasa sielewi hatma yangu"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
4h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
20h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’