Baada ya kujitambulisha na kiwango bora kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Singida United, kiungo mshambuliaji wa Yanga Bernard Morrison leo atawaongoza mabingwa hao wa kihistoria kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho la Azam raundi ya nne dhidi ya Tanzania Prisons
Mchezo huo utapigwa saa kumi jioni kwenye dimba la Taifa
Huo utakuwa mchezo wa pili kwa timu hizo kukutana msimu huu, Yanga ikishinda bao 1-0 kweye mchezo wa ligi uliopigwa mkoani Iringa
Hata hivyo mchezo wa leo utakuwa na sura tofauti kutokana na mabadiliko ya kikosi cha Yanga
Yanga itakuwa nyumbani, hivyo watataka kupata ushindi ili kuwapa furaha mashabiki wao ambao leo wanatarajiwa kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa
Lakini pia mashindano haya ni ya mtoano, ni matokeo ya ushindi pekee ambayo yataibakisha Yanga kwenye michuano
Kikosi cha Yanga kilifanya maandalizi yake ya mwisho jana kuelekea mchezo huo wa kukata na shoka
Mchezo huo unatarajiwa kuwa na upinzani mkali lakini ni lazima mshindi apatikane baada ya dakika 90 na kama hakutakuwa na mshindi basi changamoto ya mikwaju ya penati itatumika
Β