Kiraka Said Juma Makapu ameendelea 'ku-enjoy' nafasi kwenye kikosi cha kwanza baada ya kuanza mchezo wa pili mfululizo
Leo Makapu ameanzishwa katika mchezo wa kombe la FA dhidi ya Tanzania Prisons, mchezo unaopigwa uwanja wa Taifa
Mzanzibar huyo ambaye pia anamudu vyema kucheza nafasi ya kiungo mkabaji, anasimama kwenye safu ya ulinzi wa kati pamoja na Lamine Moro
Ni mabadiliko ambayo kocha Luc Eymael ameyafanya baada ya Ali Mtoni kukosekana kwa kuwa anatumikia adhabu ya kuonyeshwa kadi nyekundu mchezo dhidi ya Azam Fc
Mtoni atakosa michezo mitatu
Aidha mkongwe Kelvin Yondani ni kama amepewa mapumziko baada ya kucheza mfululizo Yanga na timu ya Taifa kwa muda mrefu
Katika michezo ya hivi karibuni, Yondani alifanya makosa ambayo yaliigharimu timu
Beki Andrew Vicent nae ameanzia benchi katika mchezo huo ambao utapigwa saa kumi jioni