Yondani amewaambia Simba watamsahau Okwi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Oct 2017
Yondani amewaambia Simba watamsahau Okwi
Beki kisiki aliyezaliwa upya katika kikosi cha Yanga Kelvin Yondani 'Cotton' amewaambia mashabiki wa Simba kuwa Jumamosi watamsahau mshambuliaji wao Emanuel Okwi kutokana na kibano atakachompa.

Yondani ameahidi kutompa nafasi mshambuliaji huyo anayeongoza orodha ya ufungaji bora akiwa na mabao nane ambayo yote ameyafunga kwenye uwanja wa Uhuru.

Yondani, Juma Abdul na Raphael Daudi hawakuwemo kwenye kikosi cha Yanga kilichopata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Stand United mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kocha George Lwandamina aliamua kuwapumzisha wachezaji hao kwa ajili ya mchezo dhidi ya Simba kwa kuwa wote wana kadi mbili za njano.

Rostand, Abdul, Gadiel, Yondani na Dante ndio chaguo la kwanza katika safu ya ulinzi ya kikosi cha Yanga.

Aidha Yondani na Dante wametengeneza pacha imara na kuwa nguzo muhimu kwenye safu ya ulinzi ya Yanga iliyoruhusu mabao matatu pekee msimu huu.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’