Morrison kuendeleza 'shibobo' kwa tahadhari

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Jan 2020
Morrison kuendeleza 'shibobo' kwa tahadhari

Kiungo mshambuliaji wa Yanga Bernard Morrison amesema anapofanya mbwembwe uwanjani halengi kuwadhihaki timu pinzani bali ni mahsusi kwa ajili ya kuwapa burudani mashabiki ambao wamelipa viingilio kuingia uwanjani

Aidha Bernard ameongeza kuwa hatafanya matukio hayo wakati wote, isipokuwa pale ambapo timu iko kwenye mazingira ya uhakika wa kuondoka na ushindi

Morrison ametoa kauli hiyo siku moja baada ya kocha Luc Eymael kueleza kutofurahishwa na matukio hayo ambayo aliyafananisha na dhihaka kwa timu pinzani

"Mashabiki wanakuja uwanjani kuona timu yao inashinda, ndio maana wanalipa viingilio, lakini ninapoona timu inaongoza vizuri huwa naona ni bora kufanya kitu ambacho kitawapa burudani zaidi mashabiki wakienda nyumbani wapate cha kusimulia zaidi," amefafanua Morrison.

"Nafikiri kocha yeyote hawezi kukubali hilo moja kwa moja, namheshimu kocha wangu (Eymael) kwa alichoniambia, lakini kwangu nafikiri kuna kitu cha ziada natakiwa kukifanya kama mchezaji, sidhani kama naweza kuacha lakini nitakuwa makini wakati gani nafanya hivyo"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’