Ipo itikadi hata wengine huamini kwamba, utambulisho wa mtanzania ni alama ya chanjo ya mwili maarufu kama ‘ndui’ ambayo inapatikana kwenye bega mojawapo la mwilini mwa binadamu.
Lakini ukizungumza habari ya soka la Tanzania, lazima uguse uwepo wa vilabu viwili vya Simba na Yanga ambavyo vimetokana na vyanzo mbalimbali ikiwemo ushirikiano wa vijana katika shughuli mbalimbali itikadi pia ikichangia kuanzishwa kwa timu hizi.
Yanga ndiyo kongwe kiumri ikiwa imeanzishwa rasmi mwaka 1935 Simba ikifuata mwaka mmoja baadaye 1936 ikiitwa Sunderland jina ambalo lilitokana na timu mojawapo ya ligi ya England wakati Yanga ilikuwa ikifahamika kwa jina la Young Africans SC ambalo ni chimbuko la jina la kimarekani.
Baadaye viongozi wa serikali walivitaka vilabu hivi kubadilisha majina yao na kutumia majina halisi ya kiafrika na kuondoka kwenye majina ya kigeni, hapo ndipo tukapata Simba na Yanga.
Vilabu hivi vimejenga upinzani mkubwa katika soka la Tanzania tangu mwaka 1936 wakati huo ikichezwa ligi ya mkoa wa Dar es Salaam (Dar es Salaam League) hadi mwaka 1965 ilipoundwa ligi ya taifa lakini hadi leo vimekuwa vikiumiza vichwa vya mashabiki lukuki wa soka ndani na nje ya nchi kutaka kujua nani ataibuka na ushindi pale vidume hivi viwili vinapokutana.
Kwa mujibu ya mazungumzo ya wazee wa zamani, wanasema upinzani wao ulitokana na vyanzo vya kibaguzi. “Yanga na Simba sio kuna upinzani, kuna uadui. Uadui na upinzani wetu umeanzia pale timu ilipogawanyika kutokana na ubaguzi, kundi moja likiwa la waarabu jingine likiwa la wamatumbi, wandengereko na wazaramoâ€.
Matokeo yoyote ya timu hizi hugusa mashabiki kwa hisia tofauti, wengine huwa na shangwe kubwa wakati upande mwingine wakilia na kupoteza fahamu.
Jumamosi, Oktoba 28 timu hizi zinakutana kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara, wanakutana kwa mara ya kwanza kwenye msimu wa 2017-2018, ukiondoa ule mchezo wa Ngao ya Jamii.
Takwimu zinaonyesha timu hizi zimekutana mara 94 kwenye michezo ya ligi kuu Tanzania bara, Yanga ikiongoza kwa kushinda mechi 35 na ikiwa imefunga magoli 103 wakati Simba mechi 26 na kufunga magoli 91 huku sare zikiwa 33.
Mchezo wa Jumamosi una upekee kwa kuwa timu zote zina alama sawa (15) Simba ikiongoza ligi kwa tofauti ya mabao.
Mshindi wa mchezo atakuwa na nafasi ya kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi.
Pia mchezo huo ni muhimu kwa kocha wa Yanga George Lwandamina ambaye amepania kupata ushindi wake wa kwanza dhidi ya Joseph Omog, kocha wa Simba.
Lwandamina ameiongoza Yanga katika michezo mitatu dhidi ya Simba ya Omog na michezo yote Yanga ilipoteza. Mchezo mmoja ulikuwa wa ligi msimu uliopita Yanga ilifungwa mabao 2-1.
Baadae zikakutana kwenye nusu fainali ya kombe la Mapinduzi Simba ikashinda kwa mikwaju ya penati. Simba ilishinda tena kwa mikwaju ya penati kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii wakati wa ufunguzi wa msimu huu.
Lwandamina amedhamiria kufuta uteja huo na hakika kwa uimara wa kikosi chake sasa, ana nafasi kubwa ya kupata ushindi kwenye mchezo wa Jumamosi.

ADVERTISE HERE