Januari 04 2020 Yanga iligoma kutumia vyumba vya kubadilishia nguo uwanja wa Taifa kutokana na harufu kali iliyokuwa inatoka kwenye vyumba hivyo
Ni katika mchezo wa kwanza wa watani wa jadi dhidi ya Simba
Pamoja na kupeleka malalamiko yao mapema kwa Bodi ya Ligi, juzi walipigwa faini kutokana na tukio hilo
Jana klabu ya Namungo Fc pia ilikacha kutumia vyumba hivyo kutokana na harufu ileile
Kocha wa Namungo Fc Natihimana Thierry alisema walilazimika kukaa nje kujihami na harufu hiyo isiyoeleweka
Huu ni mwendelezo wa malalamiko ya timu nyingi zinazocheza na Simba kwenye uwanja wa Taifa
Changamoto hiyo ilianza kwenye michuano ya ligi ya mabingwa msimu uliopita ambapo timu zote zilizokuja kucheza na Simba jijini Dar es salaam zilitoa malalamiko kama hayo
AS Vita na TP Mazembe ziligoma kabisa kutumia vyumba hivyo kama walivyofanya Namungo Fc jana
Badala ya kutatua tatizo, ni jambo la kushangaza kuona TFF inaendelea kulea tatizo hilo na zaidi inaviadhibu vilabu ambayo vinawahami wachezaji kupata madhara kutokana na harufu hiyo
Yanga walipigwa faini, bila shaka Namungo Fc nao wajiandae kulipa faini kwa kugoma kuingia vyumbani
Β