Eymael awakubali Yikpe, Molinga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Jan 2020
Eymael awakubali Yikpe, Molinga

Kocha wa Yanga, Luc Eymael amewachambua washambuliaji wake, David Molinga na Yikpe Gnamein kuwa ni wenyenye uchezaji tofauti wawapo uwanjani.

Eymael ameiongoza Yanga kuibuka na ushindi katika michezo miwili mfululizo, mmoja wa Ligi na mwingine wa Kombe la FA, alisema watu wamekuwa wakimbeza Yikpe, lakini kwake ni mshambuliaji mzuri.

“Kuna aina nyingi za washambuliaji, nadhani hapa imezoeleka kuonekana wakicheza washambuliaji wenye mambo mengi. Kazi ya mshambuliaji ni kufunga, tulimuingiza katika mchezo dhidi ya Tanzania Prisons, alifanya kazi,” Eymael amenukuliwa na Mwanaspoti.

Aliendelea kufafanua kwa kusema amekuwa akivutiwa na hesabu za mshambuliaji huyo katika kutafuta nafasi za kufunga.

“Hakuna mshambuliaji anayefundishwa kufunga, huwa ni uwezo wa mchezaji binafsi kwangu ni mfungaji mzuri.”

Eymael alisema aina ya uchezaji wa Molinga ni tofauti ni mshambuliaji mwenye uwezo wa kukaa na mpira mguuni, nguvu alizonazo zineweza kumsaidia kupita kwa wepesi katika msitu wa mabeki hata wakiwa watatu.

"Ana tabia ya upambanaji naamini ushirikiano wake na wachezaji wenzake unaweza kutusaidia kuwa na msimu mzuri. Hakuna mchezaji muhimu zaidi ya mwingine kila mchezaji amekuwa na nafasi yake"

Molinga ndiye kinara wa mabao Yanga akiwa amefunga magoli matano anayemfuatia ni Patrick Sibomana mwenye mabao manne.

Tangu amejiunga na Yanga, Yikpe ameifungia timu hiyo mabao mawili moja upande wa Ligi na lingine katika kombe la FA.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
16h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
20h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’