Kikosi cha Yanga kesho Jumapili kitashuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabili Mtibwa Sugar katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Mabingwa hao wa kihistoria wanashuka dimbani wakiwa timamu kabisa baada ya kupewa mapumziko ya wiki nzima na Bodi ya ligi kwa kile kilichoelezwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Steven Mguto kuwa waliwasahau kuwapangia mechi
Mchezo huo utakuwa wa kisasi kwa Yanga, ikikumbukwa walipoteza mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi kwa mikwaju ya penati
Hata hivyo Yanga haikutumia kikosi chake kamili kwenye michuano hiyo iliyofanyika mwezi uliopita visiwani Zanzibar na Mtibwa Sugar kuibuka mabingwa
Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema wamepata muda wa kutosha kujiandaa na mchezo huo hivyo wana matumaini ya kuondoka na ushindi
Viingilip vya mchezo huo VIP A ni Tsh 15,000/- VIP B na C ni Tsh 10,000/- wakati upande wa Mzunguuko ni Tsh 5,000/-