Watani poleni kwa pigo takatifu

Admin By Admin
β€’
28 Jun 2017
Watani poleni kwa pigo takatifu
Kwa takribani wiki kadhaa mashabiki wa Yanga wamekuwa kwenye wakati mgumu hasa kwenye mitandao ya kijamii kutokana na tambo za watani zao Simba ambao timu yao ilikuwa inasajili wachezaji asubuhi, mchana na jioni.

Baada kuibuka kwa taarifa kuwa Simba imemnasa aliyekuwa kipenzi cha WanaYanga Haruna Niyonzima, ghafla zikaibuka taarifa nyingine kuwa wamekaribia kumnasa mshambuliaji mwenye macho na nyavu Donald Ndombo Ngoma.

Kuna baadhi ya vyombo vya habari viliuaminisha Umma kuwa Ngoma tayari ameshasajiliwa na Simba huku msemaji wao akitoa matani kuwa 'Mjiandae kuchoma jezi nyingine.'

Ghafla mambo yakabadilika jana Jumanne baada ya kuibuka taarifa kutoka huko Afrika Kusini kuwa Ngoma amesaini miaka mitatu kuichezea Polokwane City.

Wale mashabiki wa Simba waliokuwa wanatamba kwenye mitandao nikawaona wanaanza kuwa wapole licha ya juzi tu kumpokea Okwi walioaminishwa kuwa mkombozi wao.

Hali ikawa mbaya zaidi ilipofika saa nne usiku pale Ngoma alipotua uwanja wa ndege wa JNIA tena akapokelewa na mabaunsa wa Yanga.

Ghafla wengi wamenuna baada ya kuthibitika kuwa Ngoma amesaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia Yanga.

Ni dhahiri Ngoma ndiye mchezaji anayeogopwa zaidi na Simba na ndio maana walitamani atue Msimbazi.

Baadhi ya vyombo vya habari viliwaaminisha kuwa Yanga 'Salio limekata' hivyo hawana uwezo wa kumbakisha Ngoma kumbe wanajidanganya.

Hakika msimu ujao watajuuta kumfahamu. Natambua walitamani kuibomoa Yanga ili iwe rahisi kwao kutwaa ubingwa lakini wanajua uwepo wa Ngoma, Tambwe na Chirwa ni habari mbaya sana kuisikia.

Combination ya hawa watu ukimuongeza na Msuva ni ya hatari sana kukutana nayo hasa pale wote wanapokuwa 'fit'

Sasa habari mbaya zaidi kwenye hiyo combination ameongezeka kijana waliomlea wenyewe Ibrahim Ajib Migomba.

Kwa kweli ni budi kuwapa pole kwani ki uhalisia watakuwa na kazi ngumu sana kutwaa ubingwa.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
21h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
22h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’