Kikosi cha Yanga kesho Jumatano kinaendelea na kampeni ya kuwania ubingwa wa ligi kuu wakiwakaribisha Lipuli katika mchezo ambao utapigwa uwanja wa Taifa
Mchezo huo utapigwa muda wa usiku kuanzia saa moja
Viingilio VIP A ni Tsh 15,000/-, VIP B na C ni Tsh 10,000/- wakati Mzunguuko ni Tsh 5,000/-
Ni mchezo ambao Yanga inahitaji kuendelea kupata matokeo ya ushindi kuelekea kuanza kwa duru ya pili ya ligi hiyo
Kocha Mkuu wa mabingwa hao wa kihistoria Luc Eymael amesema vijana wake wameiva na wako tayari kuendeleza wimbi la ushindi
Baada ya kupoteza michezo yake miwili ya mwanzo, Luc ameiongoza Yanga kushinda michezo mitatu mfululizo
ADVERTISE HERE