Timu ya Taifa imara inahitaji ligi imara - Eymael

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Feb 2020
Timu ya Taifa imara inahitaji ligi imara - Eymael

Mkufunzi wa Yanga Luc Eymael amesema ligi imara inapelekea kuwa na timu ya Taifa imara hivyo ni muhimu kwa Tanzania kuwa na ligi imara

Akizungumza baada ya mchezo dhidi ya Lipuli Fc jana ambao ulimalizika kwa Yanga kuondoka na ushindi wa mabao 2-1, Eymael amesema kuna matukio ambayo hayatoi taswira nzuri

"Tanzania mnahitaji kuwa na ligi yenye ushindani ambao baadae utatoa timu imara ya Taifa na vilabu kufanya vizuri kwenye michuano ya Kimataifa," alisema Luc

"Kwa hali ilivyo sasa malalamiko ni mengi kuwa kuna timu zinanufaika na nyingine zinaonewa, sio jambo zuri"

Aidha akizungumzia mchezo dhidi ya Lipuli, Eymael alisema mchezo huo ulikuwa wa vipindi viwili

Kipindi cha kwanza walikuwa bora na walipaswa kufunga zaidi ya mabao matatu

Lakini kipindi cha pili walipunguza kasi, jambo ambalo anadhani pengine linasababishwa na uchovu

Aidha Luc ametoa malalamiko ya harufu kuendelea kutesa wachezaji kwenye vyumba vya kubadilishia nguo

Mbelgiji huyo aliwatoa wachezaji nje ya vyumba wakati wa mapumziko

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
11h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
20h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’