KCB kumzawadia nyota wa mchezo mpambano wa Yanga na Simba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
26 Oct 2017
KCB kumzawadia nyota wa mchezo mpambano wa Yanga na Simba
Mechi ya Simba na Yanga siku zote inautamu wake hiyo ni baada ya wadhamini wenza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), wanatarajia kumzawadia Sh 500,000 mchezaji atakayeibuka nyota wa mchezo ”Man of the match” Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 15 sawa na Yanga, lakini Wekundu wa Msimbazi hao wamewazidi wenzao kwa idadi ya mabao ya kufunga, wakiwa wamecheka na nyavu mara 19, wakati watani wao wakiwa na 10.

Meneja Masoko wa Benki ya KCB Tanzania, Edgar Masato, alisema wameamua kufanya hivyo ili kuwachochea wachezaji wa timu hiyo kuonyesha kandanda la kuvutia siku hiyo.

“Tukiwa kama wadhamini wenza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, tunajiona tunajukumu la kutoa hamasa kwa wachezaji na timu kwa ujumla kuonyesha kandanda la kuvutia ili kutoa burudani inayostahili kwa mashabiki wa soka nchini na kwingineko wanakofuatilia mchezo huo wa watani wa jadi,” alisema, Masato

Alisema kuwa wanaamini, kila mchezaji atajituma kadri ya uwezo wake wote ili kuonyesha kipaji chake alichojaaliwa na Mwenyezi Mungu na mwisho wa siku kuisaidia timu yake kupata ushindi na tunaamini taratibu zote zitakazofanywa na kamati ya Tuzo ya VPL iliyopo chini ya shirikisho la mpira wa miguu nchini kwa kumpata mchezaji nyota wa mechi hiyo.

Aliwataka wachezaji wa Yanga na Simba kuwatendea haki mashabiki wa soka kwa kuonyesha kandanda la kistaarabu ambalo ndilo hasa linalowafanya mashabiki kuacha shughuli zao na kumiminika uwanjani siku hiyo.

Aliongeza: “Tunaamini kwa kufanya hivyo, tutakuwa si tu tunautendea haki udhamini wetu, lakini pia kuchangia kutoa burudani kwa mashabiki wa soka, wakiwamo wateja wetu wa KCB.”

KCB imejitosa kudhamini ligi hiyo msimu huu ikiwa ni mara ya kwanza kufanya hivyo.

Kwa hisani ya Mwananspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →