Eymael kubadili kikosi Jumanne

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Feb 2020
Eymael kubadili kikosi Jumanne

Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema kwenye ujao wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City, anatarajiwa kuwapa mapumziko baadhi ya nyota ambao wamecheza mfululizo

Akizungumza jana baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting, Eymael alisema baadhi ya wachezaji wanahitaji mapumziko

"Tumecheza vizuri kipindi cha kwanza na tulistahili kwenda mapumziko na uongozi wa kuanzia mabao matatu lakini hatukutumia nafasi nyingi tulizotengeneza. Mlinda lango wa Ruvu Shooting nae anastahili pongezi kwani aliokoa mipira mingi ya hatari"

"Kipindi cha pili tulipunguza kasi, hili ni tatizo nadhani mchezo ujao tutawapa mapumziko baadhi ya wachezaji kwani kwa jinsi ratiba ilivyo, tumekuwa tukicheza mfululizo," amesema

Tariq ndani mchezo ujao

Mshambuliaji Tariq Seif huenda akapewa nafasi ya kuongoza safu ya ushambuliaji kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City baada ya kupona majeraha

Jana Tariq alikuwa miongoni mwa wachezaji wa akiba hata hivyo hakupata nafasi ya kucheza

Eymael alifafanua kuwa kutokana na mchezo ulivyokuwa ukiendelea, aliona haikuwa sahihi kumuingiza Tariq

"Nilipanga kama tungefunga mabao mawili angeingia. Najua mashabiki wana shauku kubwa ya kumuona tangu arejee kutoka majeruhi. Lakini atakuwepo kwenye mchezo ujao," alisema kocha huyo raia wa Ubelgiji

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
4h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
8h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
13h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’