TFF yachunguza kamati ya saa 72

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Feb 2020
TFF yachunguza kamati ya saa 72

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limesema kuwa litaivunja Kamati ya Saa 72 ya shirikisho hilo kama watabaini kuna uzembe unaofanyika katika kutoa maamuzi.

Kamati ya Saa 72, ikijulikana pia kama Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi, ni chombo maalumu kilichopo chini ya TFF na Bodi ya Ligi ambacho hushughulikia masuala mbalimbali ambayo yanahusu ukiukwaji wa kanuni na sheria ambazo zinaendesha ligi zote nchini, ikiwemo ishu za wachezaji, viongozi wa timu na marefa wa ngazi zote.

Uamuzi huo unakuja mara baada ya kuibuka malalamiko kutoka kwa wadau mbalimbali wakidai chombo hicho kinachelewa kutoa maamuzi ya matukio mbalimbali yaliyotokea michezoni, huku baadhi ya matukio hayo yakishindwa kutolewa ufafanuzi licha ya kuonekana kuwa kuna makosa ya wazi yamefanyika.

Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidau, amesema kuwa wapo katika mpango wa kuichunguza Kamati ya Saa 72, ili kujua kama kuna watu hawafanyi kazi ipasavyo na kuzua malalamiko, ambapo aliongeza kuwa endapo watabaini upungufu wowote basi wataivunja kamati hiyo na kuijenga upya ili kuepusha malalamiko ambayo siyo ya lazima.

"Tunaandaa utaratibu wa kuichunguza Kamati ya Saa 72 ya Bodi ya Ligi na TFF, hii inatokana na malalamiko yaliyojitokeza hivi karibuni juu ya kuwepo kwa ucheleweshaji wa kutoa ufafanuzi juu ya matukio fulani.

"Kwa kawaida kamati hiyo hukutana kila Jumatatu ya kila wiki, hivyo tunataka tuijenge upya ili iwe inakutana kila siku baada ya mechi kuchezwa ili kuchunguza kama kuna lolote limetokea na kisha kutolea ufafanuzi na ikibidi adhabu kama kutakuwa na tukio la namna hiyo,” alisema Kidau.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
9h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’