Baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Mbeya City, kikosi cha Yange kimerejea mazoezini kujiandaa na mchezo unaofuata dhidi ya Tanzania Prisons
Mchezo huo utapigwa Jumamosi, Februari 15 kwenye uwanja wa Taifa
Huo utakuwa mchezo wa tatu kwa Yanga na Prisons kukutana msimu huu, Yanga ikishinda michezo yote miwili iliyopita
Mabingwa hao wa kihistoria walianza kwa kupata ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo wa kwanza wa ligi kisha wakapata ushindi wa mabao 2-0 kwenye mchezo wa raundi ya 32 kombe la Shirikisho
Baada ya kupunguzwa kasi na Mbeya City jana, Yanga imepania kurejesha makali yake kwenye mchezo dhidi ya Prisons
Mkufunzi wa Yanga Luc Eymael amesema wanahitaji kushinda mechi zilizo mbele yao ili kuwasogelea vinara wa ligi hiyo Simba ambao wako mbele kwa alama 16 lakini pia wakiwa wamecheza michezo miwili zaidi
Eymael amekiri haitakuwa rahisi kutwaa ubingwa lakini wana kila sababu ya kupambana ili kuhakikisha wanapata nafasi ya kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao