Uongozi wa Yanga ulifanya mabadiliko ya mpiga picha wa klabu wakimuondoa Godlisten Anderson maarufu Chicharito na kumleta Onesmo Abraham
Mchakato huo ulisimamiwa na kitengo cha habari ambacho kiko chini ya Hassan Bumbuli, Afisa Habari wa klabu ya Yanga
Hata hivyo baadhi ya mashabiki wameonyesha kutofurahishwa na mabadiliko hayo wakimtuhumu mpiga picha mpya kuwa mnazi klabu ya Simba
Machapisho yake ya kwenye mitandao ya kijamii ndio yamemuweka matatani kwani ameonyesha kuwa mnazi wa Simba

Miongoni mwa mambo ambayo mashabiki wa Yanga na hata Simba hawatakubali ni hili la mwajiriwa wa klabu kuwa shabiki wa upande wa pili
Nadhani sio suala la hapa nchini tu, hata mataifa mengine kwa timu pinzani ni hivyo
Hii ni kutokana na upinzani wa jadi ambao baadae unazaa utamaduni
Inaelezwa tayari uongozi wa Yanga umechukua hatua ambapo Mwenyekiti Dk Mshindo Msolla ameagiza ajira yake isitishwe mara moja