Changamoto safu ya ushambuliaji bado

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Feb 2020
Changamoto safu ya ushambuliaji bado

Wakati mwingine unaweza kumuelewa kocha Luc Eymael kwa nini amemfanya David Molinga kuwa mshambuliaji wake kiongozi kwenye kikosi cha Yanga

Molinga anaonekana kuwa bora zaidi ukilinganisha na washambuliaji wengine waliopo

Kukosekana kwake kwenye kipindi cha kwanza pamoja na Ditram Nchimbi aliyekuwa anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano na Haruna Niyonzima ambaye ni majeruhi, kulipunguza kasi ya Yanga kwenye mchezo dhidi ya Prisons leo

Katika mchezo huo Yanga ilimtegemea zaidi Bernard Morrison huku Tariq Seif akionekana kufanya jitihada ingawa anahitaji muda zaidi wa kucheza ili kuzoeana na wenzake

Yikpe Gnamien bado haonekani kufit kwenye mfumo wa Eymael ingawa mwenyewe anajaribu kumfanya aingie kwenye timu yake

Eymael mwenyewe amekiri kuwa safu yake ya ushambuliaji haiko sawa na alitamani kusajili mshambuliaji mwingine haraka lakini sheria za soka la Tanzania haziruhusu wachezaji huru kusajiliwa dirisha likiwa limefungwa

Timu imekuwa ikicheza vizuri kuanzia nyuma na sehemu ya kiungo, kazi inapaswa kufanywa kuiongezea makali safu ya ushambuliaji

Pengine mwishoni mwa msimu dirisha kubwa la usajili litakapofunguliwa, Yanga itarejea tena sokoni kusaka mshambuliaji

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’