Kwa kweli wajiandae kisaikolojia

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Oct 2017
Kwa kweli wajiandae kisaikolojia
Wakati Simba ikiendelea kupiga hesabu kuelekea mechi yao ya Yanga, watani zao waliojichimbia Morogoro wala hawana presha, kwani silaha ilizonazo kwa sasa kikosini zimewafanya mabosi wao kupiga miluzi ya furaha.

Kama Simba inamfikiria zaidi Ibrahim Ajib na kasi yake ya mabao, katika mazoezi ya Yanga kazi imeachwa kwa Obrey Chirwa na Pius Buswita ili kuwalaza mapema Wekundu wa Msimbazi.

Iko hivi. Yanga inaendelea na maandalizi yake Chuo cha Kibaptisti cha Biblia pale Bigwa nje kidogo ya Morogoro Yanga katika siku ya jana walikuwa wakiweka mkazo katia kufunga na kila mchezaji alionyesha uwezo mkubwa.

Kwa mazoezi jinsi yalivyofanyika unaweza kuthubutu kusema kikosi kimeipandisha mlima Simba kwa kutotabirika katika nani atawamaliza wekundu hao kutokana na sio tu ufanisi wa washambuliaji wake bali hata viungo.

Katika siku hiyo ya jana makocha wote walikuwa makini, Juma Pondamali akiwanoa makipa wake kutegua mitego ya washambuliaji George Lwandamina, Shadrack Nsajigwa na Noel Mwandila walikuwa makini kutengeneza mbinu za kufunga.

Mwiba katika safu ya ushambuliaji hakuwa Ajib peke yake, lakini hata pacha wake Chirwa na Buswita nao walikuwa hawazuiliki katika mazoezi hayo kila mmoja akifunga mara tatu lakini vurugu zao katika kutengeneza nafasi ndiyo hatari kubwa huku viungo nao Papy Tshishimbi akiwa nyuma yao katika wasumbufu.

Manji awekwa sawa

Huku mjini habari kubwa ni juhudi zilizofanywa na Baraza la Wadhamini wa Yanga ambazo wakati wowote zinamrudisha madarakani aliyekuwa Mwenyekiti wao Yusuf Manji.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga ni kwamba vigogo hao wakiongozwa na Mama Karume na Mzee Jabir Katundu jana walifanya jambo moja kubwa litakalookoa jahazi ikiwezekana hata kupandisha mzuka kwa kikosi chao baada ya kumvaa Manji na kumtaka arejee klabuni hapo haraka.

Wadhamini hao walimuweka wazi Manji kuwa hakuna aliyekubali kujiuzulu kwake na walimuacha ili amalize kesi zake na sasa wanataka kumuona anarudi katika kiti chake kuokoa mambo.

Bilionea huyo wakati wowote usishangae kusikia atakutana na kikosi cha Yanga ili kuwajaza upepo wachezaji kabla ya kukutana na Simba.

Simba na Yanga zinakutana kesho Uwanja wa Uhuru, likiwa pambano la kwanza kwa msimu huu wa Ligi Kuu Bara na la 99 tangu waanze kukutana katika ligi mwaka 1965, huku Yanga ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza pambano la mwisho Februari mwaka huu kwa kulazwa mabao 2-1.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’