Eymael kuwashushia mziki kamili Polisi Tanzania

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Feb 2020
Eymael kuwashushia mziki kamili Polisi Tanzania

Kikosi cha Yanga kiliwasili Moshi jana na kuanza maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Polisi Tanzania ambao utapigwa kesho Jumanne kwenye uwanja Ushirika

Leo Yanga itafanya mazoezi yake ya mwisho kwenye dimba la Ushirika ambalo litatumika kesho

Yanga imetua Moshi ikiwa na kikosi chake kamili ambapo kocha Luc Eymael ameahidi kuweka 'mashine' zake zote ili kuhakikisha wanapata ushindi

Mchezo uliopita dhidi ya Prisons ambao ulimalizika kwa suluhu ya bila kufungana, Eymael alifanya mabadiliko madogo ya kikosi chake akiwapa mapumziko baadhi ya wachezaj huku Haruna Niyonzima akikosekana kutokana na ugonjwa wakati Ditram Nchimbi alitumikia adhabu ya kadi tatu za njano

Habari njema ni kuwa Niyonzima amesafiri na timu Moshi wakati Nchimbi amemaliza adhabu hivyo nyota hao wanaweza kurejeshwa kikosi cha kwanza kesho kutegemea na utimamu wao

Mchezo dhidi ya Polisi Tanzania hautakuwa mwepesi hivyo Yanga itapaswa kutumia silaha zake zote ili kujiwekea mazingira mazuri ya kushinda

Polisi Tanzania inawajumuisha baadhi ya nyota waliowahi kuitumikia Yanga kama Pato Ngonyani, Pius Buswita na Matheo Anthony ambaye yuko kwenye kiwango bora sana

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
2h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
2h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
6h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
21h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’