Nahodha Msaidizi wa Yanga Juma Abdul amekiri kuwa wanapita katika wakati mgumu kutokana na matokeo ambayo wameendelea kuyapata
Hata hivyo amesema hawapaswi kukata tamaa, wanahitaji kurekebisha makosa yanayojitokeza wasonge mbele
"Kila mtihani una mitiani yake kikubwa kuwa watulivu kuangalia tunakosea wapi nakuweza kurekebisha makosa ili tuweze kusonga mbele," amesema Abdul
Yanga jana ililazimishwa sare ya bao 1-1 na Polisi Tanzania katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Ushirika, Moshi
Huo ni mchezo wa tatu mfululizo Yanga inakosa ushindi
Pia ililazimishwa matokeo ya sare dhidi ya Mbeya City na Tanzania Prisons
Ni mwenendo ambao umefifisha matumaini ya kuwania ubingwa wa ligi kuu msimu huu
ADVERTISE HERE