Manji matatani tena, akabiliwa na tuhuma za kukwepa kodi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Oct 2017
Manji matatani tena, akabiliwa na tuhuma za kukwepa kodi
Kampuni ya Udalali ya Yono (Yono Auction Mart) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Tawi la Temeke leo Oktoba 27 wamemkamata mfanyabiashara Yusuf Manji akikabiliwa na tuhuma za kutolipa malimbikizo ya kodi inayokadiriwa kufikia Tsh 300 milioni.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Yono, Scolastica Kivera alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, ambapo amesema kwamba, mbali na kumkamata Manji, pia wamefunga nyumba ya kuhifadhia mali (godown) pamoja na ofisi yake iliyopo kando ya Barabara ya Nyerere ili alipe kodi anayodaiwa na serikali.

Yono ambao ni wakala wa ukusanyaji wa madeni ya serikali kupitia TRA, wamesema kwamba wanamshauri Manji alipe deni analodaiwa ili waweze kufungua majengo yake wanayoyashikilia kwani kinyume na hapo watapiga mnada mali zilizopo ndani ya majengo kwa idhini ya TRA ili waweze kufidia deni hilo.

Kivera ameeleza kwamba, hatua ya wao kushikilia mali hizo ni kumtaka Manji alipe deni analodaiwa.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’