Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema wanawafahamu waliozusha taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii kuwa wachezaji wa timu hiyo wamegawanyika huku wengine wakiwa na madai ya mishahara
Jana Yanga ilikana kuwepo kwa tatizo la kuwalipa mishahara wachezaji wake ambapo taarifa ya timu hiyo ilisema hakuna mchezaji yeyote mwenye madai, mishahara inalipwa kwa wakati
Bumbuli amesema wanafahamu lengo la walioanzisha uzushi huo kuwa ni kutaka kuwavuruga kuelekea mchezo wa watani wa jadi ambao utapigwa March 08 kwenye uwanja wa Taifa
"Hakuna mchezaji anayedai wala hakuna mgawanyiko ndani ya timu, hiyo taarifa inayosema kuna wachezaji wanalipwa na GSM na wengine wanalipwa na klabu ni uongo mtupu. Wamedhamiria kutuvuruga kuelekea mechi yetu ya watani wa jadi mwezi ujao," amesema
Wadhamini wa Yanga kampuni ya GSM ilichukua jukumu la kuihudumia timu hiyo mwishoni mwa mwaka 2019 ambapo walianza na zoezi la kufanya usajili wa dirisha dogo
GSM pia wamemleta mtaalam wa kusimamia mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uwendeshaji wa klabu ya Yanga