Mbinu sio tatizo Yanga - Luc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Feb 2020
Mbinu sio tatizo Yanga - Luc

Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema changamoto ya timu yake kutofunga mabao katika mechi za hivi karibuni haisababishwi na mbinu anazotumia uwanjani

Tangu aanze kuinoa Yanga Eymael amekuwa akitumia mfumo 4-2-3-1 ambao anaweka viungo wengi katikati huku mbele akiweka mshambuliaji mmoja

Jana kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union, Eymael alianza na 4-4-2 lakini baadae akarejea kwenye mfumo wake wa siku zote

"Tulitumia 4-4-2 kwa dakika 20 lakini hatukupata kile tulichokuwa tunakihitaji. Mimi sipendelei sana mfumo huo lakini ilinibidi niutumie katika jitihada za kusaka matokeo," Eymael alisema baada ya mchezo dhidi ya Coastal Union uliopigwa uwanja wa Mkwakwani ambao ulimalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana

Katika mchezo huo Eymael aliwaanzisha Ditram Nchimbi na Tariq Seif pamoja lakini baadae akampeleka Nchimbi pembeni na kumuacha Tariq akiwa mshambuliaji pekee

Yanga inarejea jijini Dar es salaam leo tayari kuwakabili Gwambina Fc kwenye mchezo wa kombe la FA raundi ya tano ambao utapigwa Jumatano, uwanja wa Taifa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
2h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
18h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
23h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’