Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz ametoa ufafanuzi wa tukio liliojiri jijini Tanga juzi baada ya mchezo dhidi ya Coastal Union ambao ulimalizkia kwa suluhu ya bila kufungana
Msemaji huyo wa Yanga amesema hakuzozana na mashabiki baada ya mchezo kama ilivyoripotiwa na vyombo vingi vya habari
Kilichotokea ni kuwa aliibiwa simu na aliweza kumbaini mwizi wake na vyombo vya usalama kumtia nguvuni
"Kuna kijana aliniibia simu, ndiye aliyesababisha purukushani yote iliyotokelezea pale, mimi siibiwi kizembezembe! Nawashukuru maafisa wa Jeshi la Polisi walimtia nguvuni na kumpeleka mahala anapostahili," alisema Nugaz
"Hakukuwa na mabishano yoyote na mashabiki, tulikwenda Tanga tukiwa na lengo la kupata ushindi lakini haikuwa hivyo. Tumeachana na matokeo hayo na sasa tunajipanga kuelekea mchezo wa FA dhidi ya Gwambina"
Nugaz aliongozana na timu mkoani Tanga na tayari wamerejea jijini Dar es salaam kwa ajili ya mchezo unaofuata