Baada ya kulazimishwa matokeo ya sare katika michezo minne, jana Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Gwambina Fc na kutinga robo fainali ya michuano ya kombe la FA (ASFC)
Sasa mabingwa hao wa kihistoria watahitaji kuendeleza moto huo wa ushindi keshokutwa Jumamosi watakapowakabili Alliance Fc katika mchezo wa ligi kuu
Mchezo huo umepangwa kupigwa uwanja wa Taifa
Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema matokeo ya ushindi katika mchezo huo na ule utakaofuata March 03 dhidi ya Mbao Fc, yatawaweka katika nafasi nzuri kuelekea mchezo dhidi ya Simba ambao utapigwa March 08
ADVERTISE HERE