Kiungo mshambuliaji wa Yanga Patrick Sibomana haonekani kikosini kwenye mechi za hivi karibuni imeelezwa kuwa aliomba ruhusa kurejea kwao Rwanda kushughulikia matatizo binafsi
Sibomana ameifungia Yanga mabao manne kwenye ligi lakini tangu mabingwa hao wa kihistoria waanze kunolewa na Luc Eymael, Mnyarwanda huyo amekosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza
Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema nyota huyo aliruhusiwa kwenda kushughulikia matatizo ya kifamilia
"Alituomba aende kwao Rwanda kushughulikia pasipoti ya mkewe ambayo muda wake umemalizika," alisema
Sibomana ni miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa na Mwinyi Zahera na wameendelea kubaki kikosini
Washambuliaji Sadney Urikhob, Juma Balinya na Issa Bigirimana waliomba mikataba yao ivunjwe huku Mustafa Suleyman akiachwa dirisha dogo