Bui afafanua picha inayosambaa mitandaoni

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Feb 2020
Bui afafanua picha inayosambaa mitandaoni

Picha zinazunguka kwenye mitandao ya jamii zikiwaonyesha wachezaji wa Yanga wakihamisha vitu vyao kutoka kwenye nyumba waliyokuwa wanaishi, Kariakoo jijini Dar es Salaam lakini taarifa ikasambaa kuwa jamaa hao walitimuliwa.

Picha hizo, zinawaonyesha, Abdulaziz Makame, Adeyum Saleh, Mapinduzi Balama na wengine.

Makame ametoa ufafanuzi wa tukio hilo ambapo amesema hawakufukuzwa isipokuwa waliamua wenyewe kuhama. Bui amesema hawakufurahishwa na mazingira pamoja na kodi kubwa waliyokuwa wanaitoa.

"Mkataba wetu na Yanga ilikuwa kulipiwa miezi sita na ilipoisha, tuliamua wenyewe kuondoka kwa sababu kodi iliyokuwa inalipwa na klabu ni kubwa tofauti na uhalisia wa nyumba yenyewe na sisi hatuna uwezo wa kuilipa ndio maana tumehama kwenda kwenye nyumba tunayoweza kumudu kulipa kodi," Bui aliiambia Mwanaspoti

Bui slitaja gharama ya nyumba ambayo Yanga iliwalipia ni 4 milioni, ambapo sasa wametafuta nyumba nyingine nzuri ambayo gharama yake ni nafuu zaidi

Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema ni utashi wa wachezaji wenyewe kuamua kuhama walipokuwa wamepangiwa na timu kwenda kuishi mahali pengine

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
10h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
14h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
19h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
22h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’