Kuna uwezekano mkubwa mshambuliaji wa Yanga Bernard Morrison ataukosa mchezo dhidi ya Simba ambao utapigwa March 08 kwenye uwanja wa Taifa
Nyota huyo alipelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF kufuatia tukio la kumpiga kiwiko mchezaji wa Prisons katika mchezo wa ligi kuu uliomalizika kwa suluhu ya bila kufungana mapema mwezi huu
Lakini mpaka leo Kamati ya Nidhamu bado haijakutana, taarifa za chinichini zimedai kuwa kamati hiyo itakutana wakati wowote
Adhabu ambayo Morrison anaweza kupewa kama atapatikana na hatia ni kufungiwa michezo mitatu
Yanga imebaki na michezo miwili dhidi ya Alliance Fc na Mbao kabla ya kucheza na Simba March 08
Morrison huenda akajadiliwa sambamba na kiungo wa Simba Jonas Mkude ambaye pia amepelekwa kamati ya nidhamu
Nyota wote wawili wanaweza kuukosa mchezo wa watani wa jadi