Mwezi wa pili ulikuwa mzuri sana kwa mlinda lango wa Yanga Metacha Mnata kwani katika mechi nane alizokaa langoni, ameruhusu mabao mawili tu huku akipata cleansheet sita
Jana kwenye mchezo dhidi ya Alliance Fc Metacha alidhihirisha ubora wake kwa kuokoa mashambulizi kadhaa ya hatarai langoni kwa Yanga na kuwahakikishia mabingwa hao wa kihistoria kuondoka na cleansheet ya ushindi wa mabao 2-0
Ni bahati mbaya tuzo hizi za kila mwezi zimekuwa zikiwabagua sana walinda lango lakini kwa hakika Metacha alistahili kupewa tuzo hiyo kwa mwezi wa pili
Kwa sasa Metacha anaonekana kuaminiwa zaidi na kocha Luc Eymael mbele ya Mkenya Farouk Shikhalo akianza katika mechi tatu zilizopita
ADVERTISE HERE