Nchimbi ajiwekea malengo ya kufunga mabao zaidi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Mar 2020
Nchimbi ajiwekea malengo ya kufunga mabao zaidi

Baada ya juzi kufunga mabao mawili kwenye mchezo dhidi ya Alliance Fc, mshambuliaji wa Yanga Ditram Nchimbi amesema atahakikisha anafunga mabao mengi zaidi katika michezo iliyobaki

Kabla ya mabao yake ya juzi, Nchimbi hakuwa ameifungia Yanga tangu alipojiunga nayo mwezi Januari 2020

Hata hivyo changamoto hiyo inaweza kuwa ilichangiwa na uamuzi wa kocha Luc Eymael kumbadilishia majukumu na kumtumia nafasi ya winga

Juzi alimrudisha nafasi ya mshambuliaji wa kati na hakufanya makosa kwani dakika 45 za kipindi cha pili alizopewa zilimtosha kuihakikishia Yanga ushindi muhimu

"Nimesajiliwa Yanga kwa ajili ya kufunga mabao licha ya kwamba nacheza na ninaweza nikafanya majukumu mengine makubwa, watu wanataka kuona nazitikisa nyavu, hilo linanifanya nipambane kwa kadri ninavyoweza ili kutimiza malengo yangu," amesema.

"Hakuna mshambuliaji asiyependa kuwa na mabao mengi, binafsi natamani uwepo wangu utambulike kwa wadau wa soka kwa kuzitikisa nyavu, sijakata tamaa nitapambana niwezavyo, naamini nitafunga sana tu kwa mechi zilizosalia"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
51m ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
1h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
4h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
19h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
23h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’