Leo Yanga imeshinda mchezo wake wa tatu mfululizo ikimaliza changamoto ya kutoka sare mechi nne mfululizo
Ni kama ule msemo wa aliyewahi kuwa msemaji wa Yanga Jerry Muro kuwa ameleta password ya ushindi, umeanza kudhihiri baada ya ushindi wa leo
Ukiondoa mchezo wa FA dhidi ya Gwambina Fc ambao ulikuwa na presha kubwa, Yanga ilicheza vizuri sana mchezo dhidi ya Alliance Fc na hata leo kwenye mchezo dhidi ya Mbao Fc licha ya mabadiliko makubwa ya kikosi
Katika michezo hiyo miwili, Yanga imeupiga mpira mwingi, ile kampa-kampatena ya miaka ya nyuma imeanza kuonekana
Ni dhahiri mwendo huu wa Yanga umeanza kuzitia hofu timu zinazokuja kupambana na mabingwa hao wa kihistoria
Mchezo unaofuata ni dhidi ya Simba. Ushindi kwenye mchezo huu utafufua matumaini ya kuwania ubingwa msimu huu
Hata hivyo kesho Simba itacheza na Azam Fc, mchezo ambao matokeo ya sare au ushindi kwa Azam Fc yanaweza kuipa faida Yanga