Sibomana aweka malengo ya mabao 10 msimu huu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Mar 2020
Sibomana aweka malengo ya mabao 10 msimu huu

Kiungo mshambuliaji wa Yanga Patrick Sibomana amesema kuwa ataendelea kupachika mabao kila atakapopewa nafasi na kocha Luc Eymael

Baada ya kukosekana kwa wiki kadhaa, Sibomana jana alirejeshwa kwenye kikosi cha kwanza katika mchezo dhidi ya Mbao Fc ambapo alifunga bao la pili na kuihakikishia Yanga ushindi wa mabao 2-0

Hilo lilikuwa bao lake la tano msimu huu

Akizungumza baada ya mchezo huo, Sibomana alisema lilikuwa jambo la faraja kwake kurejea kikosini na kufanikiwa kuifungia Yanga

Aidha nyota huyo kutoka Rwanda amesema amejiwekea malengo ya kufunga angalau mabao 10 msimu huu

"Kuifungia timu mabao ni jukumu langu, hivyo nitahakikisha nafunga kila nitakapopewa nafasi ya kucheza. Kwa msimu huu nimejiwekea malengo ya kufunga mabao 10 au zaidi. Bado mechi zipo nyingi, malengo hayo naweza kuyatimiza

Kuhusu nafasi ya kucheza ni jukumu la mwalimu kupanga nani acheze, muhimu nitahakikisha nafanya vizuri ili niendelee kupewa nafasi ya kucheza," alisema Sibomana

Tangu kutua kwa Eymael, Sibomana amepoteza nafasi kwenye kikosi cha kwanza lakini pia ujio wa Bernard Morrison umechangia

Morrison amekuwa akifanya vizuri winga ya kushoto ambayo mara nyingi Sibomana hucheza

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
5h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
9h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
13h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
14h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’