Nchimbi atamani aingie 'super-sub' mchezo dhidi ya Simba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Mar 2020
Nchimbi atamani aingie 'super-sub' mchezo dhidi ya Simba

Mshambuliaji wa Yanga, Ditram Nchimbi, amesema anataka kuanzia benchi kwenye mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mshambuliaji huyo aliyetua Yanga usajili wa dirisha dogo akitokea klabu ya Polisi Tanzania, amesema mara nyingi amefanya vizuri akitokea benchi kwani huwa anakuwa tayari ameusoma mchezo

"Kwangu huwa naona nafanya vizuri ninapotokea benchi na kwenda kubadili mchezo, ninapokuwa nje mara nyingi nausoma mchezo na nikiingia ninakuwa na jukumu la kufanya timu yangu iwe bora zaidi," amesema Nchimbi

"Siwapangii benchi la ufundi kikosi au namna ya kunitumia lakini kwa sababu wote tunahitaji matokeo ya ushindi katika mechi na Simba lakini nikianzia benchi nina uhakika nitafanya mambo makubwa nikiingia"

Nchimbi ameifungia Yanga mabao mawili na pia akitoa pasi mbili za mabao. Mafanikio hayo aliyapata katika mechi zote ambazo alianzia benchi

Haitashangaza kama kocha Luc Eymael atamtumia kama super-sub kwenye mchezo huo ambao utaanza saa 11 jioni

Mcongoman David Molinga ambaye alikosa mchezo wa duru ya kwanza huenda akaanza kwenye mchezo huo sambamba na Tariq Seif Kiakala

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
56m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
21h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’