Dogo shabiki wa Yanga Twalib Kimbwembwe kutoka wilayani Kilwa mkoa wa Lindi ambaye hivi karibuni video yake ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii akifanya uchambuzi wa mchezo wa leo dhidi ya Simba, amepokelewa na uongozi wa Yanga jijini Dar es salaam
Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz alifanya jitihada za kumpata 'dogo' huyo baada ya kuiona video yake kupitia Azam TV
Pamoja na kuushukuru uongozi wa Yanga kwa kumpa nafasi ya kushuhudia mbashara mchezo wa leo, Twalib ametabiri kuwa leo Yanga itashinda mabao 2-0
ADVERTISE HERE