Baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba jana, siku ya Alhamisi, March 12 kikosi cha Yanga kitashuka uwanja wa Taifa kumenyana na KMC katika mchezo ambao KMC watakuwa wenyeji
Mchezo huo utapigwa kuanzia saa kumi jioni badala ya saa moja iliyopangwa awali kwa kile kinachoelezwa marekebisho ya hitilafu ya umeme uwanja wa Taifa
Baada ya mchezo huo Yanga itaelekea mkoani Lindi kuifuata Namungo Fc tayari kwa mchezo ambao utapigwa March 15 katika uwanja wa Majaliwa wilayani Ruangwa
ADVERTISE HERE