Rais wa Shirikisho la soka nchini Jamal Malinzi leo amepandishwa kizimbani Mahakama ya Kisutu jijini Dar es salaam akikabiliwa na mashitaka ya matumizi mabaya ya ofisi.
Sambamba na Malinzi, Katibu Mkuu wa TFF Celestine Mwesigwa nae anakabiliwa na mashitaka sawa na Malinzi.
Nao viongozi wawili wa Simba, Rais Evance Aveva na Makamu wake Godfrey Nyange 'Kaburu' nao wamepandishwa kizimbani wakikabiliwa na mashitaka matano likiwemo la utakatishaji wa fedha.
Kesi ya Aveva na Kaburu itatajwa tena Julai 13 na viongozi hao waandamizi wa Simba watabakia rumande hadi tarehe kesi yao iatakapotajwa tena kwa kuwa makosa ya utakatishaji fedha hayana dhamana.
Aidha Malinzi na Kaburu wanaowania nafasi za uongozi katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Agosti 12, wamezuiwa kwenda kuhudhuria 'interview' ya mchujo wa wagombea.

ADVERTISE HERE