Bosi wa zamani Simba akiri Tshishimbi ni habari nyingine

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
30 Oct 2017
Bosi wa zamani Simba akiri Tshishimbi ni habari nyingine
Katibu Mkuu wa zamani wa Simba Mwina Kaduguda ‘Simba wa Yuda’ amekubali uwezo wa kiungo wa Yanga Papy Kabamba Tshishimbi raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kutokana na uwezo mkubwa aliouonesha kwenye mechi ya Yanga vs Simba Jumamosi ya October 28, 2017.

Kaduguda amesema ukiwa na wachezaji watatu wenye uwezo kama wa Tshishimbi timu yako inacheza mashindano ya Afrika kwa raha.

“Kuna mtu mmoja hatari sana mimi nimemkubali anaitwa Tshishimbi, yule jamaa kila mpira unapotua yupo ana nguvu, stamina na pasi zake zina macho anapiga popote anapotaka. Alikosa magoli baada ya kupiga mikwaju miwili, ukiwa na wachezaji watatu kama wale unacheza kombe la klabu bingwa Afrika kwa raha”-Kaduguda.

“Lakini vilevile kulikuwa na Buswita pamoja na Raphael Daud walikata eneo la kiungo na kuwafunika wachezaji wa Simba eneo la kiungo ni sawa na injini.”

Kaduguda amesema viongozi wa Simba hawapaswi kujivunia kuwa na pesa na wachezaji wa gharama kwa sababu pesa pekeake hajiwahi kuleta ubingwa.

“Viongozi wasiridhike na uwezo wa kipesa, pesa pekeyake haijawahi kuleta mafanikio bila kuwa na wataalam kwa mfano kuwa na benchi la ufundi. Kitu cha msingi kama Simba wanataka ubingwa wanatakiwa kuwa wamoja, Simba imekosa ubingwa kwa muda mrefu kwa sababu wameuacha umoja.”

Kwa hisani ya ShaffihDauda
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →