Eymael ataja siri ya kuifunga Simba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Mar 2020
Eymael ataja siri ya kuifunga Simba

Baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya watani zao Simba, Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael amesema matokeo hayo mazuri waliyopata yalitokana na kufanyia kazi mapungufu ya kikosi cha Simba

Bao pekee katika mchezo huo lilifungwa na Bernard Morrison, ambaye alimtungua kipa wa Simba, Aishi Manula kwa mpira wa adhabu uliozama wavuni baada ya kuchezewa rafu na Jonas Mkude nje kidogo ya eneo la 18.

Eymael amesema alikuwa akiwafuatilia wapinzani hao mara kadhaa walipokuwa wakicheza na kufanyia kazi ubora na mapungufu ya kikosi chao.

Eymael amebainisha kuwa kitu alichofanikiwa ni kuidhibiti safu ya kiungo ambayo mechi zake tatu zilizopita, Simba ilicheza vizuri ikiongozwa na Mzambia Clatous Chama na Mkenya Francis Kahata.

"Vijana wangu wamecheza vizuri, wamefanyia kazi yale yale tuliyokuwa tukifanya mazoezini na kufanikiwa kupata pointi tatu muhimu katika mchezo wetu huu dhidi ya Simba, ila haikuwa mechi rahisi," alisema Eymael.

Mbelgiji huyo alisema baada ya matokeo hayo, wanaenda kujipanga kwa mara nyingine kwenda kutafuta pointi tatu muhimu katika mchezo wa ligi hiyo unaofuata dhidi yaKMC.

"Nina furaha na kumshukuru Mungu kwa kupata ushindi dhidi ya Simba, hatukucheza kama 'dabi', tulicheza kama fainali, ingawa tulipoteza nafasi kadhaa, kama ile ya Nchimbi (Ditram) na Kaseke, lakini tutaendelea kupambana kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye michezo iliyobaki.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
8h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
12h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
13h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
13h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
17h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’