Azam Fc imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo ambao umepigwa uwanja wa Uhuru
Ushindi huo umeifanya Azam Fc iendelee kusalia nafasi ya pili baada ya kufikisha alama 54
Hata hivyo mabingwa hao wa kombe la FA msimu uliopita, wamecheza mechi tatu zaidi ya Yanga inayoshika nafasi ya tatu ikiwa na alama 50
Yanga itashuka dimbani Alhamisi kumenyana na KMC
Nao Namungo FC wamelazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Biashara United hivyo kubaki katika nafasi ya nne wakiwa na alama 49
Aidha mchezo kati ya Polisi Tanzania dhidi ya Mtibwa Sugar umeahirishwa baada ya maji kujaa kwenye uwanja wa Ushirika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha Moshi
Matokeo ya mechi zote zilizopigwa leo;

ADVERTISE HERE