Kiraka Said Juma Makapu ni miongoni mwa wachezaji saba wa Yanga walioitwa kuunda timu ya Taifa inayojiandaa na michezo ya kusaka tiketi ya fainali za kombe la dunia dhidi ya Tunisia na michuano ya CHAN ambayo itafanyika Cameroon mwezi ujao
Tangu aanze kutumika kama mlinzi wa kati ya kocha Luc Eymael, kiwango cha Makapu kimeimarika sana na kocha Etienne Ndayiragije amefanya uamuzi sahihi kumjumuisha kwenye kikosi chake
Hii ni nafasi kwake kuimarika zaidi na pengine kujitengenezea mazingira ya kupata nafasi ya hata kwenda kusakata kabumbu nje ya nchi
Lakini pia, mafanikio yake yawe chachu kwa nyota wengine, hakuna kukata tamaa kwani kila mmoja ana wakati wake
Kama Makapu angekata tamaa Yanga pengine leo jina lake lingekuwa limepotea kwenye soka la Tanzania
Ni mchezaji aliyetua Yanga tangu mwaka 2014, akisajiliwa na Hans Van Der Pluijm
Tangu wakati huo hakuwa na nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza lakini hakuchoka kupambana na leo matunda yake ameyaona