Mapema leo Group la WhatsApp la 'Yanga for life', likiwakilishwa na msanii wa filamu nchini, Vicent Kigosi, ‘Ray’, wametoa zawadi ya fedha, viatu na ‘shin guard’, kwa wachezaji watatu, waliofanya vizuri katika michezo ya Ligi.
Straika Ibrahim Ajib, alikabidhiwa kiasi cha Tsh Milioni moja, baada ya kuibuka nyota wa mchezo kwenye mechi mbili za Kagera na Stand United.
Papy Kabamba Tshishimbi, aliyechagulia nyota wa mchezo wa ‘Derby’, dhidi ya Simba, amekabidhiwa Tsh 500,000 huku kipa Youthe Rostand, akipata Tsh 200,000, viatu na ‘shin guard’.
Akizungumza baada ya kukabidhi zawadi hizo, Ray amesema kama mashabiki wa Yanga wameanzisha utaratibu huo ili kuwapa motisha wachezaji kuhakikisha timu inafanya vizuri zaidi msimu huu.
Aidha, Ray amewakaribisha WanaYanga wote ambao watapenda kujiunga kwenye group la WhatsApp la Yanga For Life wawasiliane nao kupitia 0717 554545.
Utaratibu huu ni wa kupongezwa na hakika sasa matunda yake yameanza kuonekana.
Wachezaji wengine ambao wamenufaika na utaratibu huu wa kutuzwa baada ya kuibuka wachezaji bora ni Kelvin Yondani na Pius Buswita.

ADVERTISE HERE