Nahodha wa Yanga Papy Tshishimbi amesema walichelewa kupata taarifa ya mchezo wao dhidi ya KMC kuhamishiwa uwanja wa Uhuru jambo ambalo amesema kwa kiasi fulani liliwavuruga
Hata hivyo Tshishimbi amewapongeza KMC kwa kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya mabingwa hao wa kihistoria
Akizungumza baada ya mchezo huo, Tshishimbi amesema walijitahidi kupambana ili wapate ushindi lakini hawakuwa makini kutumia nafasi walizopata
"Kufungwa ni matokeo ya mchezo, tulitahidi kucheza vizuri na kutengeneza nafasi nyingi lakini hatukuzitumia wenzetu wamepata nafasi moja wakafunga"
"Ni mchezo ambao tumeshtukizwa kwani taarifa ya mchezo kupigwa uwanja wa Uhuru tumeipata leo, kwa kiasi fulani jambo hili limetuvuruga kisaikolojia"
"Tumekubali matokeo, tunawapongeza KMC kwa kupata ushindi. Sisi tunajipanga na mchezo wa Jumapili dhidi ya Namungo Fc," alisema Tshishimbi