Morrison aingiza mamilioni Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Mar 2020
Morrison aingiza mamilioni Yanga

Mshambuliaji wa Yanga, Benard Morrison ameiingizia Yanga Sh.30 milioni, baada ya jezi zake kuuzwa kama njugu kwenye mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga uliopigwa Machi 8 Jijini Dar es Salaam.

Nyota huyo anayetamba kwa sasa na kukubalika ndani ya Wanajangwani hao, anakuwa mchezaji mwenye mauzo makubwa zaidi ya Yanga kwenye miaka ya karibuni

Lakini vilevile tafsiri nyepesi ni kwamba mauzo hayo yana uwezo wa kulipa posho za mechi tatu zijazo za ushindi Yanga ambazo kila wakishinda wanapewa Sh. 10 milioni.

Mhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema mchezaji huyo aliongoza kwa mauzo ya jezi baada ya jezi zake 1,500 kuuzwa katika mchezo huo aliofunga bao pekee dakika ya 44.

Nugaz alisema katika mauzo hayo ya Sh 20,000 ambayo ilikuwa bei elekezi inayoendelea wiki nzima Yanga ilipata mapato hayo na bado inaendelea kuuza jezi ya nyota huyo.

"Awali tuliandaa jezi 1,000, wakaja watu wanaoomba tuwatengenezee jezi ya huyu mtu, tukaziandaa nyingine 500 na zote ziliisha. Jezi ya pili kwa mauzo ilikuwa ni ya Tshishimbi, kwani naye kabla ya mchezo huo tuliuza zaidi ya jezi zake 400," alisema Nugaz

Aliongeza kuwa wachezaji wengine ambao jezi zao zinauliziwa zaidi ni Ditram Nchimbi na Mapinduzi Balama

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’