Umeusikia mkwara wa Pluijm

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Nov 2017
Umeusikia mkwara wa Pluijm
Licha ya kukiri kwamba tangu aondoke klabu ya Yanga amekuwa na mahusiano mazuri na timu yake hiyo ya zamani, Hans van Pluijm kocha wa Singida United amesema Jumamosi atahakikisha anaiadhibu vikali Yanga.

Pluijm amesema siku hiyo hataruhusu ukaribu wake na Yanga uathiri ndoto yake ya kuipa ushindi timu yake, SIngida United.

Pluijm amesema mchezo huo ni wa kipekee kwa sababu utachezwa katika uwanja wao wa nyumbani kwa mara ya kwanza tangu kuanza msimu huu kutokana na kumalizika kwa matengenezo yake.

"Asilimia kubwa ya wachezaji wa Yanga nimesajili mimi na hata mafanikio waliyokuwa nayo mimi ndiyo chanzo, lakini hayo yalishapita mimi nimfanyakazi wa Singida United hapa ndipo ambapo napata riziki ya kuendesha familia yangu hivyo nimejiandaa kuhakikisha tunashinda mchezo huo ili kujiweka katika mazingira mazuri kwenye msimamo,"amesema Pluijm.

Kocha huyo raia wa Uholanzi, amesema anatambua kuwa Yanga, ni timu kubwa na nzuri lakini hata kikosi chake nacho siyo kibaya kwani katika mechi nane walizocheza wameonyesha mabadiliko na kuzoea ushindani uliopo kwenye ligi.

Amesema anafurahia kukutana na Yanga kipindi hiki ambacho tayari wachezaji wake wa kigeni wameanza kuzoea ligi, na ameahidi kutoa upinzani mkubwa kwa mabingwa hao watetezi wa taji la ligi kuu siku hiyo ya Jumamosi.

Singida chini ya Pluijm na msaidizi wake Jumanne Chale, inashika nafasi ya tano kwenye msimamo ikiwa na pointi 13.

Jumamosi Novemba 04 inakutana na Yanga ambayo imeboreka zaidi ikiwa imeshinda michezo miwili kati ya mitatu iliyopita.

Singida United ilicheza mchezo wa kirafiki na Yanga wakati wa maandalizi ya msimu mpya ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-2 mchezo ukipigwa dimba la Taifa.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
2h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
10h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
11h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’